Numbers 1

Watu Wahesabiwa Kwa Mara Ya Kwanza

1 a Bwana alisema na Musa katika Jangwa la Sinai, katika Hema la Kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri. Akamwambia, 2 b“Hesabu watu wa jumuiya yote ya Waisraeli kwa kufuata koo zao na jamaa zao, ukiorodhesha kila mwanaume kwa jina lake, mmoja mmoja. 3 cWewe na Haruni mtawahesabu kwa migawanyo yao wanaume wote katika Israeli wenye miaka ishirini na kuendelea ambao wanaweza kutumika katika jeshi. 4 dMwanaume mmoja kutoka kila kabila, kila aliye kiongozi wa jamaa yake, atawasaidia. 5 eHaya ndiyo majina ya wanaume watakaowasaidia:

“kutoka Reubeni, ni Elisuri mwana wa Shedeuri;
6 fkutoka Simeoni, ni Shelumieli mwana wa Surishadai;
7 gkutoka Yuda, ni Nashoni mwana wa Aminadabu;
8 hkutoka Isakari, ni Nethaneli mwana wa Suari;
9 ikutoka Zabuloni, ni Eliabu mwana wa Heloni;

10 jkutoka wana wa Yusufu:
kutoka Efraimu, ni Elishama mwana wa Amihudi;
kutoka Manase, ni Gamalieli mwana wa Pedasuri;
11 kkutoka Benyamini, ni Abidani mwana wa Gideoni;
12 lkutoka Dani, ni Ahiezeri mwana wa Amishadai;
13 mkutoka Asheri, ni Pagieli mwana wa Okrani;
14 nkutoka Gadi, ni Eliasafu mwana wa Deueli;

15 okutoka Naftali, ni Ahira mwana wa Enani.”

16 pHawa walikuwa wanaume walioteuliwa kutoka jumuiya, viongozi wa makabila ya baba zao. Walikuwa wakuu wa koo za Israeli.

17Musa na Haruni wakawachukua wanaume hao waliokuwa wamepewa majina yao, 18 qwakaita jumuiya yote pamoja katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili. Watu wakaonyesha nasaba zao kwa koo zao na jamaa zao, nao wanaume waliokuwa na miaka ishirini au zaidi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, 19 rkama Bwana alivyomwagiza Musa. Hivyo aliwahesabu katika Jangwa la Sinai:

20 sKutoka wazao wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli:
Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
21 tIdadi kutoka kabila la Reubeni ilikuwa watu 46,500.

22 uKutoka wazao wa Simeoni:
Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi walihesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
23 vIdadi kutoka kabila la Simeoni walikuwa watu 59,300.

24 wKutoka wazao wa Gadi:
Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
25 xIdadi kutoka kabila la Gadi walikuwa watu 45,650.

26 yKutoka wazao wa Yuda:
Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
27 zIdadi kutoka kabila la Yuda walikuwa watu 74,600.

28 aaKutoka wazao wa Isakari:
Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
29 abIdadi kutoka kabila la Isakari walikuwa watu 54,400.

30 acKutoka wazao wa Zabuloni:
Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
31 adIdadi kutoka kabila la Zabuloni walikuwa watu 57,400.

32 aeKutoka wana wa Yusufu:
Kutoka wazao wa Efraimu:
Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
33 afIdadi kutoka kabila la Efraimu walikuwa watu 40,500.

34 agKutoka wazao wa Manase:
Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
35Idadi kutoka kabila la Manase walikuwa watu 32,200.

36 ahKutoka wazao wa Benyamini:
Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
37 aiIdadi kutoka kabila la Benyamini walikuwa watu 35,400.

38 ajKutoka wazao wa Dani:
Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
39 akIdadi kutoka kabila la Dani walikuwa watu 62,700.

40 alKutoka wazao wa Asheri:
Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
41 amIdadi kutoka kabila la Asheri walikuwa watu 41,500.

42 anKutoka wazao wa Naftali:
Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
43 aoIdadi kutoka kabila la Naftali walikuwa watu 53,400.

44 apHawa walikuwa wanaume waliohesabiwa na Musa, Haruni na viongozi kumi na wawili wa Israeli, kila mmoja akiwakilisha jamaa yake. 45 aqWanaume wote Waisraeli waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi la Israeli walihesabiwa kufuatana na jamaa zao. 46 arJumla ya hesabu yao ilikuwa watu 603,550.

47 asHata hivyo, jamaa ya kabila la Lawi hawakuhesabiwa pamoja na wengine. 48Bwana alikuwa amemwambia Musa: 49 at“Kamwe usihesabu kabila la Lawi wala kuwaweka pamoja katika hesabu ya Waisraeli wengine. 50 auBadala yake, waweke Walawi kuwa viongozi wa Maskani ya Ushuhuda, juu ya samani zake na kila kitu kilichomo ndani yake. Wao watabeba Maskani na samani zake zote; wataitunza na kupiga kambi kuizunguka. 51 avWakati wowote Maskani inapohamishwa, Walawi wataifungua, na wakati wowote maskani inapotakiwa kusimamishwa, Walawi watafanya kazi hiyo. Mtu yeyote mwingine ambaye atasogea karibu nayo atauawa. 52 awWaisraeli watapiga mahema yao kwa makundi makundi, kila mwanaume katika kambi yake mwenyewe chini ya bendera yake. 53 axHata hivyo, Walawi watapiga mahema yao kuzunguka Maskani ya Ushuhuda ili ghadhabu isiipate jumuiya ya Waisraeli. Walawi watawajibika kwa utunzaji wa Maskani ya Ushuhuda.”

54Waisraeli walifanya yote haya sawasawa kama Bwana alivyomwamuru Musa.
Copyright information for SwhKC